Yanga imetwaa ubingwa wa kombe shirikisho

Klabu ya soka ya Yanga, imetwaa ubingwa wa
kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
maarufu kama Kombe la Azam Sports
Federation Cup (ASFC) kwa kuichapa Azam, kwa
mabao 3-1.
Mchezo huu uliopigwa kwenye uwanja wa taifa
jijini Dar es salaam, ulishudia kikosi cha Yanga,
ilipata ushindi wake kupitia kwa magoli ya
mshambuliaji Amisi Tambwe aliyefunga bao la
kwanza katika dakika ya tisa ya kipindi cha
kwanza kisha akaongeza bao la pili katika dakika
ya 47 ya kipindi cha pili.
Katika dakika ya 81 winga Deus Kaseke,
alihitimisha kazi kwa kufunga bao la tatu baada
ya kuunganisha krosi ya Simon Msuva.Bao la
kufutia machozi la Azam,liliwekwa kambani na
mshambuliaji Didier Kavumbagu.
Licha ya Yanga kushinda mchezo huu wa fainali
Azam ndio wataiwakilisha Tanzania katika
michuano ijayo ya kombe la shirikisho huku
Yanga wakiwakilisha katika michuano ya klabu
bingwa Africa.

No comments