Kenya yawasaka wasukiwa wa Islamic State
Polisi nchini Kenya inaendelea na msako wa
kuutia mbaroni mtandao wa kundi la wapiganaji
linalojiita Islamic State ambalo linataka kukita
mizizi yake nchini Kenya kwa lengo la kufanya
mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi
wasio kuwa na hatia. Hayo ni kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi.
Kauli hiyo imetolewa baada ya polisi nchini
Kenya kuwatia mbaroni watu wawili
wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la
wapiganaji la IS.
Kwa mujibu wa polisi, kukamatwa kwa wawili
hao ambao ni Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo
Mohammed kumezuia mashambulizi ya kigaidi
yaliyokuwa yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na
silaha nyingine katika mji wa Nairobi na
Mombasa.
Mbali na kukamatwa kwa washukiwa hao wawili,
polisi pia imepata vitu mbalimbali katika nyumba
ya Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri,
waya na mbolea ambazo inadaiwa zingetumika
kutungezea bomu la nyumbani.
Polisi imeendelea kusema, katika uchunguzi
wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo na
Abubakar ni miongoni mwa waandishi wa makala
iliyokuwa inasambaa kupitia mtandao ambao
ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba
katika eneo la Afrika Mashariki ambalo
limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa ISIS
Abubakr Al-Baghdadi.
No comments