Hukumu kesi ya shambulio la Al-Shabab Uganda

Mahakama mjini Kampala leo inatarajiwa kutoa
hukumu katika kesi ambapo wanaume 13
wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya
mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab mwaka
2010.
Watu zaidi ya 70 walifariki kwenye mashambulio
hayo yaliyotekelezwa watu wakitazama fainali ya
Kombe la Dunia la mwaka 2010.
Kesi hiyo imechukua miaka sita.
Baadhi ya washtakiwa walikuwa wameambia
mahakama kwamba waliteswa na maafisa wa
ujasusi wa kanda, Marekani na Uingereza.
Lakini mahakama ya kikatiba nchini Uganda
ilifutilia mbali madai hayo.
Washtakiwa 13
Washukiwa ni 13 kutoka Uganda, Kenya na
Tanzania. Saba ni Waganda, 5 Waenya na mmoja
anatoka Tanzania.
Wao ni: Bw Habib Suleiman Njoroge, Isa Ahmed
Luyima Abubaker Betamatory na Dkt Ismail
Kalule.
Wengine ni Suleiman Hijar Nyamandondo, Hassan
Haruna Luyima, Hussein Hassan Agade, Bw Idris
Magondu, Mohamed hamid Suleiman na Yahya
Suleiman Mbuthia.
Kutokea kwa shambulio
Shambulio lilifanyika 11 Julai, 2010 na vituo viwili
vilishambuliwa Ethiopian Village Restaurant,
Kabalagala na Kyadondo Rugby Club, Nakawa
watu waliopokuwa wamekusanyika kutazama
fainali ya Kombe la Dunia iliyokuwa ikichezewa
Afrika Kusini.
Idadi ya wahanga
Watu 74 walifariki katika shambulio hilo na
wengine 70 kujeruhiwa. Takriban watu 60
waliouawa ni wa kutoka Uganda. Wengine
waliofariki dunia ni kutoka mataifa ya Ethiopia,
Eritrea, India na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo pamoja na mmoja kutoka Ireland na
Marekani.
Kuendeshwa kwa kesi
Kesi ilianza miaka mitano baadaye baada ya
kucheleweshwa na hatua ya washukiwa kupinga
kupelekwa kwao nchini Uganda na kudai kuteswa
na vikosi vya usalama.
Lakini Oktoba 2014 mahakama ya kikatiba
ilitupilia mbali kesi yao na hivyo kesi kuanza.
Wanashtakiwa makosa ya: ugaidi, mauaji na
kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.
Jaji wa mahakama kuu aliyesikiliza kesi hiyo ni
jaji Alfonso Owiny Dollo.
Mwendesha mashtaka kuuawa
Wakati mmoja muongoza mashtaka aliuawa na
watu wasiojulikana waliokuwa na bunduki.

No comments