Sekta 5 Zinazoongoza Kwa Uchumi na Ajira Tanzania, Bilioni 15 Kudili na Tatizo la Ajira

Tunae Waziri Jenista Muhagama ambaye wizara yake inadili na ishu mbalimbali zikiwemo ajira, kazi na vijana ambapo anaelezea mambo makubwa matatu yafuatayo kuhusu sekta zilizoonekana kutoa ajira kwa wingi lakini pia na tatizo la ajira na wanavyodili nalo kwenye mpango mpya. 


1: ‘Sekta ya Kilimo, sekta ya miundombinu barabara na ujenzi ya aina mbalimbali, sekta ya viwanda, sekta ya Mahoteli, Viwanda, mafuta na gesi, sekta ya maswala ya IT ndio zinazoongoza kwa uchumi na kutoa ajira, sasa serikali baada ya kugundua hivyo kwenye bajeti mwaka huu kama wizara tumetenga Bilioni 15 tutazitumia kuwafundisha vijana wetu waweze kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye soka la ajira’ – Jenista Muhagama 



2: ‘Sasa hivi tutakua na mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka Tanga kwenda Uganda, litakapokua linatengezwa kutakua na ajira nyingi kwahiyo sisi lazima tuwatayarishe vijana wetu wa Tanzania, ni ngazi ngapi za ajira zitatakiwa? wakihitajika mafundi wa kuchomea mabomba ni lazima tuwatayarishe vijana wetu wakapate ajira, Mameneja na ajira nyingine, tunaendelea pia kutazama makundi mbalimbali ya vijana hasa Wahitimu wetu ili wapatiwe namna nzuri ya kujiajiri’ 



3: ‘Tuna program maalum kabisa wa kuwachukua vijana wetu kwa mujibu wa sheria lakini kwa kujitolea kwenda jeshini (JKT) na wanapokwenda kule wengi wanachukuliwa na taasisi zetu za ulinzi na usalama lakini wengi wanabakia, tumeanza kuwafundisha Walimu wa JKT wawe wanawafundisha na ujasiriamali ili wakitoka hapo waweze kujiajiri kama kufungua kampuni zao za ulinzi na usalama’

No comments