Sishikani mkono na mtu nisiye na mazoea naye – Diva

Diva doesn’t shake hands. Hivyo ukikutana naye halafu ukampa mkono akaukaushia, habari ndiyo hiyo.


Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Diva amesema hiyo ni moja ya sababu inayomfanya watu wasema anajisikia.

“Mfano artist anaweza akaja akanipa mkono and I say like ‘no I don’t shake hands, I will tell you I don’t shake hands. Sishikani mkono na mtu nisiye na mazoea naye,” anasema. “Ukinisalimia sikujui, sikujibu.”

Anasema mmoja wa watu aliowahi kuwafanyia hivyo ni Hussein Machozi ambaye aliwahi kumsalimia na kumpa mkono lakini akakataa.

Sikiliza kipindi cha Chill na Sky hapo chini.

No comments