Lemonade ya Beyonce yatabiriwa kuuza kopi laki 5 katika wiki ya kwanza
Queen Bey anarudi kwenye chat. Album yake mpya, Lemonade inatarajiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200.


Kwa mujibu wa Billboard, album hiyo inaweza kuuza kopi 500,000 na zaidi ya units za 700,000 za hadhi ya album kwenye wiki yake ya kwanza. Lemonade ilitoka April 23 baada ya kuoneshwa documentary mahsusi ya album hiyo kwenye kituo cha runinga, HBO.
Album hiyo inapatikana Tidal, iTunes na Amazon. Kopi za kawaida zitaingia sokoni May 6.
Album hiyo imepokolewa vizuri huku Rolling Stone, wakiipa nyota 5. “LEMONADE is her most emotionally extreme music, but also her most sonically adventurous,” limeandika jarida hilo.
Kwa sasa Beyonce yupo kwenye ziara ya dunia ya Formation.
No comments