Hatutaki Leicester City watangazie ubingwa OT – Ander Herrera
Mchezaji wa timu ya Manchester United, Ander Herrera amekiri kuwa Leicester City wanastahili kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza lakini siyo kwenye uwanja wa Old Traford.

Leicester City ambayo inaongoza ligi wakiwa na pointi 76, inatakiwa kushinda mchezo wake wa ugenini siku ya Jumapili dhidi ya Manchester United ili watangazwe kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo.
Akiongea na Sky Sports, Herrera alisema, “Sote tunaifikiria Manchester United, bado tumo kwenye mbio, ni lazima tuwe katika nne bora kwani ni muhimu sana kwetu. Baada ya hayo ni kweli kwamba tunacheza dhidi ya Leicester, kikosi bora na mahiri sana. Lakini hatutaki watwalie ubingwa Old Trafford – Nadhani wanastahili kutwaa ubingwa lakini watauchukulia kwao.”
“Sisi ni Manchester United na ni lazima tushinde kwa sababu tunahitaji kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Leicester wanaweza kutwaa ubingwa Old Trafford. Tutapambana hadi sekunde ya mwisho kupata nafasi nne bora,” aliongezea Herrera.
No comments